Tuesday, August 28, 2012

MSANII SISQO AUMBUKA NCHINI UGANDA

Mwanamuziki wa R&B wa kundi la Dru Hill la Marekani, Sisqo, juzi ameambulia za uso jijini Kampala, Uganda baada ya show yake kuhudhuriwa na watu wasiozidi 1,000 kwenye uwanja unaochukua watazamaji 20,000.

Mahudhurio hayo yametokana na uzito wa show yenyewe na kushuka kwa umaarufu wa Sisqo.

Maumivu hayo yamekuja wiki moja tu baada ya show ya mwanamuziki wa Jamaica Demarco iliyoambulia mahudhurio kiduchu pia.

Pamoja na kula za uso, Sisqo na mwanamuziki wa Ghana mwenye wimbo wa Azonto walitoa show nzuri iliyosaidiwa na music systems ya nguvu.

Wasanii wa Uganda waliosindikiza show hiyo ni pamoja na Leila Kayondo, Bobi Wine, Jackie Chandiru AK47 na Jose Chameleone.

Kwa mujibu wa vyanzo nchini Uganda, mahudhurio kwenye show hiyo yalikuwa hafifu kutokana na uchumi mbaya kwa wananchi wengi ambao wamejikuta bila hela ya kufanyia starehe.

“You know what is going on. People do not have money. Very few can pay Shs 25,000 to attend a show these days. When a show is at 25,000, you need a minimum of Shs 40,000 and that is if you are alone. Remember at the concert, you have to drink and eat something,”shabiki mmoja aliuambia mtandao wa hipipo.com.
Bobi Wine Jackie Chandiru
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!