Wednesday, August 1, 2012

MSHINDI WA GARI YA PILI APATIKANA KATIKA DROO YA MWISHOYA KAMPENI YA VUMBUA DHAHABU CHINI YA KIZOBO.

Mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti bw.Stephen Gannon ( kushoto ) akiongea na waandishi wa habari alipohudhuria kwa mara ya kwanza droo ya mwishon ya promosheni ya Vumbua Hazina Chini ya Kizibo iliyoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti tangu mwezi wa tano 2012 hadi leo. Kulia ni Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni hiyo Bi Teddy Mapunda.
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw Ephraim Mafuru (kushoto) akiongea na mmoja wa washindi katika droo hiyo ya mwisho kwa njia ya simu ya kiganjani.(katikati) ni meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo na kushoto ni wasimamizi na wakaguzi kutoka bodi ya taifa ya  michezo ya kubahatisha.


=====  ======  ====== ======.

MSHINDI WA GARI YA PILI APATIKANA KATIKA DROO YA MWISHOYA KAMPENI YA VUMBUA DHAHABU CHINI YA KIZOBO.

August 01, 2012 Dar Es Salaam: Imekuwa ni desturi kwa wateja, wadau, wapenzi na watanznia wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya Serengeti kutega masikio ya na kutenga muda wao mwingi kusikiliza redio, kutazama tuninga na kusoma kupitia kwenye magazeti na mtandaoni juu ya nani kajishindia nini kati ya zawadi zinazotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL iliyokuwa ikiendelea tangu ilipoanza 2/05/2012 mpaka leo 01/08/2012 inapofikia tamati yake.

Katika kipindi chote hicho, watanzania wengi wamekuwa wakifurahia kuwa watumiaji wakubwa wa bidhaa ama vinywaji vinavyozalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti hasa vinywaji vile vilivyoainishwa katika promosheni hiyo kutokana na kufululiza kutokea kwa washindi mbalimbali waliojishindia zawadi zikiwemo Gari mpya, bajaj, pikipiki jenereta pamoja pesa taslimu.

 Asubuhi ya leo promosheni hiyo ilifika tamati katika  ofisi za CMC Motors jijini Dar es Salaam ambao ndio wauzaji na wasambazaji wa gari aina ya FORD FIGO lililopo kwenye promosheni hiyo ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ kwa kuchezesha droo ya mwisho kabisa.Droo hiyo kama ilivyo ada, ilipata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.

Awali akimkaribisha mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw.Steve Gannon anayechukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Richard Wells   na baadaye kuongea na waandishi wa habari katika mara baada ya kuchezesha droo hiyo ya mwisho mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru amesema zawadi nyingi zimekuwa zikienda kwa washindi wengi nchini kote. 

Amewashukuru sana wateja na watanzania kwa ujumla kutokana na mwitikio na ushirikiano wao mzuri waliouonyesha katika kipindi chote cha promosheni hiyo. “Kwa niaba ya kampuni ya bia ya Serengeti nachukua fursa hii kuwashukuru sana tena sana wateja wetu na watanzania wote kwa ushirikiano wao mzuri waliotupa katika kipindi chote cha promosheni na kwamba tunatambua uwepo wao katika shughuli zetu zinazoendelea” alisema Mafuru huku akiongeza kuwa mwisho wa promosheni hii ni mwanzisho wa promosheni zingine nyingi.

Kwa upande wake mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo Bw. Steve Gannon amesema amefurahishwa sana na jinsi kampuni hiyo inavyofanya kazi yake hasa inavyotekeleza sera zake za kuwa karibu na wateja wake bila kubagua, “Nimefurahishwa sana na jinsi kampeni hii maalum inayolenga kubadilisha maisha ya watanzania kwa ujumla. Hata kama tumefikia mwisho wa kampeni hii, naomba watanzania wote wajue kwamba kuna promosheni nyingi sana za aina hii ambazo tutaendeleza na kuendelea kuinua maisha ya watanzania kwa ujumla.   ” alisema Gannon.

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni  ya “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’, nchi nzima kwa muda  wa miezi kumi na Promosheni hiyo imeweza kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!