Tuesday, August 14, 2012

MTOTO AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI KIGAMBONI LEO
MTOTO mmoja ambaye hakufahamika jina lake, amefariki dunia katika ajali ya gari eneo la Kigamboni Machava leo wakati gari hilo likitokea Mji Mwema kuelekea Kivukoni. 

Ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo lenye namba za usajili T 645 AVG kufunga breki ghafla kutokana na gari lililokuwa mbele yake nalo kusimama ghafla hivyo kusababisha gari hilo kuingia mtaroni na kupoteza uhai wa mtoto huyo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!