Friday, August 31, 2012

MUIGIZAJI MAARUFU WA NIGERIA AMUUA MKEWE KWA SUMU


Rich Oganiru

Kwa watazamaji wa filamu za kinaijeria, sura ya Rich Oganiru si ngeni machoni.

Ni muigizaji maarufu wa filamu hizo na tayari ameshaigiza zaidi ya filamu 300.

Kwa mujibu wa jarida la National Enquirer la Nigeria, Oganiru anakabiliwa na kesi nzito ya mauaji ya mke wake mfanyabiashara bilionea aliyekuwa akiishi Abuja.

Huyo hakuwa mke wake wa kwanza kwani mke wake wa awali naye alikufa katika mazingira yasiyoeleweka miaka kadhaa iliyopita.

National Enquirer limedai kuwa muigizaji huyo alikuwa akiishi maisha duni kabla ya kukutana na mwanamke huyo mfanyabishara aliyebadilisha maisha yake.

Inadaiwa kuwa baada ya kifo cha mke wake aliyezaa naye watoto wawili wa kiume, alijikuta katika maisha magumu kiasi cha kukosa hata hela kununua chakula na ndipo alipokutana na mwanamke huyo aliyemwimbisha na kueleweka hasa kutokana na sura yake kuwa maarufu kwenye filamu.

Ripoti inasema kuwa baada ya kuishi pamoja na kuoana na mwanamke huyo, Rich alianza kulalamika baada ya mkewe kushindwa kushika mimba.

Inaendelea kudai kuwa mke wake alimwamini na kumfanya awe mmiliki wa baadhi ya mali zake na kuwa mwamuzi wa mambo ya kifedha kwenye kampuni yake.

Baadaye Rich aliingiwa na tamaa na kuanza kuwa na uhusiano na msichana mdogo aitwaye Iyake.


Ilikuja kugundulika kuwa mke wake anashindwa kupata mimba kwasababu alikuwa akisimbuliwa na tatizo la Fibroid.

Rich anadaiwa kumshawishi mke wake akafanyiwe upasuaji wa kuondoa tatizo naye akakubali.

Ripoti inasema mke wake alifariki muda mfupi baada ya upasuaji huo kwa madai kuwa Rich alimtembelea hospitali na kumpa kidonge bila ruhusa ya daktari kwa kudai kuwa kidonge hicho kingempunguzia maumivu bila kujua kuwa ilikuwa sumu.

Baada ya daktari kubaini kuwa mikono yake ilikuwa salama aliagiza kufanyike uchunguzi kwa mwili wa mwanamke huyo na ukabaini kuwa alipewa sumu.

Sumu hiyo ilionesha kuwekwa katika muda ambao mume wake alikuwa amekwenda kumsalimia kabla ya kufariki mke wake.

Muigizaji huyo alikuja kukiri kumuua mke wake baada ya kupokea mateso makali kutoka kwa polisi.

Hivi sasa Rich anashikiliwa kwenye kituo cha polisi mjini Abuja wakati mwili wa mke wake ukiwa mortuary.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!