Tuesday, August 28, 2012

MWANA FA ATARAJIWA KUTOA BURUDANI YA NGUVU KATIKA FAINALI ZA SHINDANO LA FREESTYLE LA NOKIARapper wa Tanzania, Hamis Mwinjuma aka MwanaFA anatarajiwa kutumbuiza kwenye fanaili za shindano la freestyle la kampuni ya simu Nokia liitwalo Nokia Don’t Break the Beat.


Fainali hizo zitafanyika Jumamosi hii ya September 1 jijini Nairobi, Kenya pande za Club Ichonic (zamani Club Barn) kuanzia saa 2 usiku huu.


Wasanii wengine watakaotumbuiza ni Bamboo, Keko, Madtraxx, Octopizzo na STL.


Mshindi wa kwanza kwenye shindano hilo atajishindia shilingi milioni 5 za Tanzania.


Pamoja na zawadi hiyo mshindi wa kwanza atakula shavu la kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Decimal Media/Universal Records.


Mkataba huo utamfanya mshindi arekodi nyimbo na kufanya video tatu katika kipindi cha mwaka mmoja huku kwenye video moja akifanya collabo na rapper wa kike Stella Mwangi, STL.


Tangu mwezi uliopita msako wa kumpata mkali wa michano Afrika Mashariki umeendelea kwa kuzunguka kwenye miji ya Nairobi, Mombasa, Kisumu, Eldoret, Kampala na Dar-es-Salaam.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!