Wednesday, August 22, 2012

NIKKI MBISHI AWAPONDA "KIGOMA ALL STARS"


Mradi wa Kigoma All Stars na wimbo wao Leka Dutigite ulipokelewa kwa pongezi nyingi nchini kiasi cha kuvutia mikoa mingine kutaka kufanya hivyo.

Lakini kadri muda unavyoenda watu wengi wameanza kuchoshwa na nia ya baadhi ya mikoa kufikiria kufanya kile kile walichofanya Kigoma.

Hata hivyo habari zinadai kuwa tayari wasanii wa Morogoro wakiongozwa na Afande Sele wamesharekodi wimbo wao chini ya jina la ‘Morogoro All Stars’.

Kwa upande wa rapper Nikki Mbishi ameamua kufunguka na kusema yake ya moyoni jinsi anavyoichukulia Kigoma All Stars.
Kupitia Facebook ameandika,  
“Tunakoendea kila mkoa wasanii watatoka na wimbo unaosifia mkoa wao: Bongo bwana vya kufanya vimeisha sasa, ila waanzilishi wa maswala ya ukabila wa mikoa Tanzania si mnawajua?.

 Hatukatai kuwakilisha ila sio kujifanya nyie ndo mnaumiliki muziki au mnaujua sana!!!
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!