Friday, August 17, 2012

“NIMEHAMIA DAR RASMI KUTAFUTA SOKO LA MUZIKI WANGU” – BABY J


MSANII kutoka visiwani Zanzibar ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye muziki kizazi kipya Baby J, amedai kuwa ameamua kuhamia jijini Dar, kwa sababu ya kutafuta soko kwani visiwani bado muziki haujukua nafasi kubwa kama ilivyo Dar.

Kauli ya msanii huyo inaweza kuwa sawa na mwezake
AT, ambaye amehamia rasmi dar kwa kufuata soko na kwa upande wa Baby J, alidai kuwa anaamini kadri siku zinavyozidi kwenda muziki wake unazidi kukua.

Msanii huyo alisema kuwa haoni sababu ya kutowashukuru mashabiki wake wa Visiwani na Bara kwa kumpa sapoti katika kila wimbo ambao amekuwa akitoa.


Hata hivyo alidai kuwa soko la muziki la Dar linamfanya aweze kutengeneza ngoma zenye ubora kwani kuna ushindani mkubwa sokoni tofauti na visiwani.


“Dar nimekuja kufanya muziki na kuchukua nafasi hivyo naamini sapoti kubwa ninayopata kutoka mashabiki ndiyo inayonipa nguvu ya kuendelea kufanya kazi hivyo nawaahidi wale wote wanaopenda kazi zangu ni kwamba sitawaangusha kabisa,”
aliongeza.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!