Sunday, August 5, 2012

NYWELE NI MUHIMU KATIKA KUFANYA MAPENZI....CHANGAMKA SHOST, UTAACHWA!!!


Sina uhakika kwanini Mungu alituumba jinsi alivyotuumba kwamba kichwa na “vikorombwezo” vyake ambavyo ni Nywele, Macho, Masikio, Pua, Madomo(kinywa, meno, ulimi n.k), Mikono na Viganja na vidole, Matiti, Tumbo, Mapaja, Miguu na Nyayo.


Hivi viungo huwa tunavitumia kila siku au mara kwa mara (kwa wale wanaojua kucheza na kuitumia vilivyo miili ya wapenzi wao) wakati tunafanya mapenzi na cha kushangaza huwa tunavitumia kufuata “mtiririko” wake yaani kama vilivyo pangwa iwe kuanzia juu kwenda chini au chini kwenda juu.

“Vifaa” hivi humpa mpenzi raha Fulani ya kimapenzi na vilevile humuongezea hamu ikiwa vitatumiwa vizuri . Ikiwa unafahamu umuhimu wake ktk kufanya mapenzi nakupongeza na nitahitaji nyongeza ya maelezo yako na ikiwa hujui basi endelea kuwa  nami ili tujifunze sote….Leo  nitazungumzia juu  ya nywele tu.
 

NYWELE:
Nywele ni sehemu muhimu sana ya urembo wa mwanamke kama ilivyo sehemu nyingine za mwili wake na wakati huohuo nywele hizo zinachukua nafasi kubwa ktk mapenzi na huongeza raha na mvuto kwa mpenzi wako hasa kama mnatoana jasho wakati mnafanya mapenzi.


Nywele za mwanamke hupendeza zaidi machoni kwa mwanaume/mpenzi wako mara baada ya kufanya mapenzi kuliko zinavyokuwa mara baada ya kutoka kwa “hairdresser/Salon”.


 Mwanaume hufurahia kucheza na kichwa cha mwanamke nakuhisi ule mkwaruzo wa nywele, harufu yake asilia iliyochanganyikana na mafuta, sabuni au “shampoo” (hivyo hakikisha hupaki mafuta yenye harufu kali kichwani).

Inasemekana wanaume wengi hupenda kushika kichwa cha mwanamke wakati wa kufanya mapenzi au kuchezeana na hukosa raha fulani ikiwa watawekewe mipaka kuwa wasiguse kichwa kwa vile wataharibu mtindo wa nywele uliogharamia “Salon”.

Sina shaka umeshawahi kusikia baadhi ya wanaume wakilalamika kuwa hawapendi wake/wapenzi wao wavae “wigs” kitandani kwa vile wanashindwa kucheza na vichwa vyao, sina hakika na wale wanawake wanaoondoa nywele zote kichwani.

Mwanamke na nywele  za mpenzi wake:
Si wanawake wote tunavutiwa na nywele za vichwani mwa wanaume bali huvutiwa na nywele sehemu nyingine za mwili kama vile kwapani, usoni (nyusi, ndevu n.k ), kifuani, sirini na kwingineko .

Mimi binafsi navutiwa sana na nywele za usoni (zinanifanya nihisi niko na Real man) na zile za miguuni hasa wakati natoa “massage” ya miguu kwa mpenzi, ule mkwaruzo wake hunipa raha ya ajabu inayonifanya nifurahie kufanya ninachokifanya kwa wakati huo ambacho ni kumkanda miguu yake, vilevile napenda kucheza na zile za sirini wakati tunaongea .

Hebu niambie na wewe unavutiwa/furahia nywele za mpenzi wako? za wapi hasa na huwa unazitumia/chezea vipi?

IRENE....
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!