Friday, August 24, 2012

OMOTOLA AJIPANGA KUANZISHA "REALITY TV SHOW"
Muigizaji wa kike wa nchini Nigeria Omotola Jalade Ekehinde yupo kwenye mpango wa kuwa na reality TV show yake nchini Nigeria.


Omotola ambaye ni miongoni mwa waigizaji waliofanikiwa zaidi kwenye tasnia ya filamu nchini humo anadaiwa kuwa kwenye mkakati wa kuwa na show hiyo iliyopewa jina la ‘The Real Omotola’.


Kuna taarifa kuwa tayari yupo kwenye hatua za kushoot show hiyo ambayo itaanza kuruka baada ya miezi miwili nchini Nigeria na Uingereza.


Show hiyo itakuwa ikionesha maisha yake ya kila siku na kuonesha mambo mengi ambayo watu wengi hawayafamu kutoka kwake.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!