Saturday, September 1, 2012

PICHA: GADNER G HABASH ALIPOTAMBULISHWA RASMI TIMES FMMtangazaji na mjasiriamali Gardner G. Habash jana ametambulishwa rasmi katika kituo cha Radio Times FM na kumaliza uvumi uliokuwa umeanza kuenea wa wapi Gardner anaelekea, baada ya kuwa nje ya kazi kwa takriban miaka miwili baada ya kujiuzuru kazi ya utangazaji katika msimu wa mwisho wa mwaka wa 2010.Hafla ya kumtambulisha mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha Radio ya Clouds FM kwa waandishi wa habari ilifanyika katika kiota cha chakula, vinywaji na burudani ya luninga za michezo City Sports Lounge ambapo Mtangzaji Scholastica Mazura ambaye ndiye mhariri mkuu wa habari katika Radio Times Fm alimtambulisha.

Gardner atakuwa akitangaza kipindi kinachoitwa Maskani ambacho kitakuwa kinaruka hewani kuanzia majira ya saa kumi alasiri mpaka saa moja usiku kuanzia siku ya Jumatatu ya Tarehe 3 Mwezi wa Tisa.

Monalisa Na Mama yake ambao nao ni watangazaji wa kipindi cha Filominata kinachorushwa siku za jumapili
Waandishi Wa Habari Wakipata Chakula Gardner akipozi pamoja na watangazaji wenzake wa Times FM Schola na Natasha Gradner akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Gardner akipozi na Kipi Malecela
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!