Friday, August 17, 2012

POLE MASANJA MKANDAMIZAJI KWA KUFIWA NA MDOGO WAKO....

 
Mchekeshaji maarufu wa kundi la Original Comedy Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji jana amefiwa na mdogo wake.

Kupitia Facebook aliandika, “ndugu nimefiwa na mdogo wangu. Tunaaga Amana kesho halafu tunaelekea kijijini kuzika. Mniweke katika maombi yenu.”

Mdogo wake aitwaye Valle Mgaya alifariki nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam na taarifa zinadai kuwa marehemu alikutwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwake.

Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Amana.
Mtandao  huu  unampa pole Masanja kwa msiba huo na Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!