Wednesday, August 1, 2012

PROF MWANDOSYA ATINGA BUNGENI LEO

Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki Profesa MARK MWANDOSYA amerejea Bungeni Mjini Dodoma ikiwa ni zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja tangu awe nje ya Bunge kutokana na kupatiwa matibabu nchini India.

Profesa MWANDOSYA ambaye pia ni Waziri asiye na Wizara Maalumu amerejea Bungeni leo na kutoa shukrani zake kwa Watanzania wote na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais JAKAYA KIKWETE alimsisitiza kwenda kutibiwa kutokana na kuona kuwa suala la afya ni muhimu.

Pia amewashukuru Wabunge wa vyama vyote vya siasa na kusema kuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa yeye kupona haraka kutokana na kwamba katika kipindi chote alichokuwa akiuguwa walionesha umoja wao kwa kumfariji bila kujali itikadi za vyama.

Katika shukrani zake pia ameitaka jamii kutambua kuwa suala la afya ni muhimu kwani bila afya hawataweza kutekeleza majukumu mbalimbali ya kujileta maendeleo.

Profesa MWANDOSYA pia ametoa rai kwa Wabunge kupima afya zao mara kwa mara hata baada ya kustaafu Ubunge kwani wasihadaike na hali waliyonayo hivi sasa ya kujiona wazima kutokana na kukaa Bungeni muda mwingi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!