Saturday, September 1, 2012

RAILA ODINGA KUWATUMIA JAGUAR NA PREZZO KWENYE KAMPENI ZA URAISI


Prezzo na waziri mkuu Raila Odinga walipokutana hivi karibuni

Mwamko wa wanamuziki vijana kujiingiza kwenye siasa haupo Tanzania pekee. Kenya mambo ni yale yale pia. Miongini mwa wasanii walioonesha dalili za kupanda kwenye majukwa ya kisiasa nchini humo ni Prezzo na Jaguar. 

Siku chache baada ya kuwasili nchini Kenya, Prezzo alipata fursa ya kukutana na waziri mkuu Raila Odinga kwa mazungumzo ya siri. 
 
Hakuna anayejua walizungumza nini lakini wengi wanaamini Raila aliutumia mkutano huo kumpongeza kwa kuiwakilisha nchi yake kwenye BBA na kumpa dondoo kadhaa za namna ya kuwa mwanasiasa aliyefanikiwa.Mazungumzo hayo yalimalizika kwa wote kupiga picha ya pamoja

Jaguar na Raila Odinga hivi karibuni
Haujapita muda mrefu, Jaguar naye akamzukia Raila ofisini kwake. Huenda ikawa ni tukio la siku moja kwakuwa Raila anaonekana kuwa na suti na tai ile ile. Jaguar na Prezzo wanaweza wasigombee uongozi wowote kwenye uchaguzi ujao, lakini wameanza kujiweka karibu na manguli wa siasa ya Kenya ili kujisafishia njia mapema.

Kwa haraka haraka, kinachokuja akilini mwetu hapa ni kuwa labda Raila Odinga anataka kuwatumia wasanii hawa wote kwaajili ya kumpigia kampeni kwenye uchaguzi ujao wa urais nchini humo.

Wote wakiwa kwenye kambi moja, kuna mvuto mkubwa utakaoonekana kwenye kampeni ya Raila hasa ukizingatia kuwa wasanii hawa walikuwa maadui wakubwa.

You never know, pengine kuna mpango wa kufanyika ngoma ya pamoja ya wakali hawa itakayompigia debe mgombea huyo wa urais. Muda utaongea.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!