Sunday, August 5, 2012

SABABU ZINAZOWEZA KUMFANYA MWANAMKE ASHINDWE KUFIKA KILELENIKukeketwa (Female Genital Mutilation).
Kukeketwa ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake. Katika Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya. 

Ingawa wanawake waliokeketwa huweza kurudia hali ya kuweza kufika kileleni, walio wengi huathiriwa sana na hiki kitendo na kuwasababishia kushindwa kufika kieleleni.

 Dini, jadi na utamaduni:
Kuna baadhi ya mitazamo na malezi ya dini, jadi au tamaduni huwapa wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na maana kuhusiana na tendo la ndoa.

Katika dini, jadi, na tamaduni nyingi ukiacha jando na unyago, elimu ya mwanamke kuhusu mwili na uzazi havifundishwa wala kutamkwa matokeo yake wanawake wengi hawaijui miili yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa kiume anamuoa binti hajui chochote kuhusu mwili wa huyo mwanamke na mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu mwili wake mwenyewe, akiguswa chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya mtoto, hapo utategemea afikishwa kileleni kweli?

 Kisaikolojia.
Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.

Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.) 

Hofu labda ya kuachwa, mashaka, kutojiamini, kukasirika, donge moyoni, kisirani au mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke kutofika kileleni, Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na kupata hisia halisi (sensations). 

Kuwa na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa Mawazo hasi (Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchomvu  kutamfanya mwanamke asifike kileleni.

 Kibailojia
Kama vile kuwa na mfumo ovyo wa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya viungo vya uzazi pia huchangia. Anaweza kuwa na uvimbe au kisukari pia huchangia. pia hitilafu za viungo baada ya kufanyiwa upasuaji hasa sehemu ya uke.

 Umri (Menopause)
Kuna wakati mwanamke kuanzia miaka 48 – 52 hupata mabadiliko ya upungufu wa homoni na huo upungufu husababisha sehemu ya uke kuwa kavu wakati wa tendo la ndoa. 

Kuwa na uke mkavu huchangia katika ufanisi wa tendo la ndoa kuwa mdogo na hatimaye kushindwa kufika kileleni.

 Si kweli kwamba mwanamke akizeeka uwezo wa tendo la ndoa unakuwa mdogo, muhimu ni kutumia vilainisho kama gel au KY jelly na libeneke linaendelea kama kawaida.

 Kutumia madawa (Medicaments).
kama unatumia dawa za kuzuia msongo wa mawazo pia huchangia ile hamu ya tendo la ndoa (libido) na matokeo yake kukosa kufika kileleni. 

Pia kuna dawa za uzazi wa mpango hupunguza hamu ya tendo la ndoa hasa zile ambazo huingizwa mwilini (sindano). Pia dawa za kupunguza pressure hupunguza uwezekano wa kufika kileleni.

 Pombe, madawa ya kulevya na sigara, Alkoholi na madawa ya kulevya hupunguza sana hamu ya tendo la ndoa. Huathiri mfumo wa Fahamu unaohusika na mzunguko wa hisia za mapenzi kati ya ubongo na uke.

 Kama inavyoathiri (alkoholi) mwanaume kudindisha vilevile huathiri mwanamke kufika kileleni. Mwonekano, urembo na umaridadi:

Kwa mwanamke jinsi anavyoonekana na jinsi mwanaume anavyoonekana kuna sehemu katika hisia za mapenzi (emotions na feelings).

Kama yeye mwenyewe anajijua kwamba hayupo vizuri kimwonekano (urembo, usafi, harufu) na pia kama mwanaume hayupo sawasawa basi anakuwa ameathirika sana kiasi ambacho hawezi kufika kileleni.

Pia wanawake wana uwezo mkubwa kunusa harufu kuliko mwanaume hivyo harufu yoyote mbaya kwake huwezi kumpeleka nje kabisa ya njia ya kwenda kileleni.

 Mazingira
Kama eneo au chumba mlichopo hakina usalama kama vile anahisi mtu anachungulia au anaweza kuingia, kwa mwanamke hiyo ni issue kwani hawezi kufika kileleni kwa sababu ya usalama wake.

Je kuna jinsi ya kuondoa tatizo la kutofika kileleni?
Kujiruhusu mwenyewe kupenda tendo la ndoa na zaidi kupenda kufika kileleni kwa hamu kubwa.

Kuwa responsible kwa mambo yote yanayohusu ufanisi wa tendo la ndoa.

Kujipa elimu na maarifa kuhusu elimu ya mapenzi kwa mwanaume na mwanamke, viungo vinavyohusika na kila kitu kinachiweza kukupa tofauti katika ufanisi uimarishaji wa tendo la ndoa kama unavyosoma hapa sasa hivi.

Kuwa na mawasiliano wakati wa tendo la ndoa hasa kuhusiana na maeneo yote ambayo unasisimka pale ukiguswa au kuchezewa.

Kufanyia kazi kila tatizo lolote la kisaikolojia na kupata solution kabla ya tendo la ndoa.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!