Saturday, August 11, 2012

SAKATA: JE KUNA MWENYE PINGAMIZI NDOA HII ISIFUNGWE?Kulikuwa na sarakasi katika kanisa la Nairobi Pentecostal Valley Road wakati shughuli ya kufungishwa ndoa kwa maharusi ilipovurugwa.

Walionuia kukitia kitumbua mchanga ni watu waliodai kuwa bwana harusi hapaswi kufunga ndoa kwa kuwa amekwepa majukumu yake kwengineko.

Waliofika na madai hayo ni mama mmoja na bintiye na kijana mwingine mmoja waliodai kuwa bwana harusi huyo, ambaye ni Kasisi alikuwa ana kasoro za kiunyumba. 

Hata, hivyo kama Lolani Kalu wa kituo cha NTV, Kenya anavyoarifu kwenye video iliyopachikwa hapo chini, walalamishi hao walitoka nje ya Kanisa na harusi ikaendelea, lakini baada ya kadhia na fedheha.

VIDEO

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!