Monday, August 20, 2012

SHILOLE NA SKENDO YA KUTEMBEA NA VIJANA WADOGO: HUWAHONGA PESA ILI AWANASE


STAA wa filamu na muziki wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anadaiwa kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kupenda uhusiano wa kimalavidavi na vijana wadogo a.k.a Serengeti boys anaowazidi umri.

Mpekuzi imedokezwa  kuwa mwanadada huyo alikuwa akifanya siri lakini sasa imevuja kwamba amekuwa akibanjuka na damu changa mfano ukitolewa kwa wasanii wenye  umri mdogo ambao aliwahi kujilainisha kwao kwa kuwahonga visenti na kuwapa gari lake watembelee ‘tauni’.

Baada ya kuzitia habari  hizo , mpekuzi ilimnyatia Shilole na  kumuuliza  kama  analolote  la  kudema, ndipo akatanua kinywa:

“Ninavyojua mapenzi hayachagui umri mkubwa wala mdogo, nawashangaa hao wanaosema hivyo, sasa wanataka niwe na wazee? Mimi ni kijana, lazima niwe na uhusiano na vijana wenzangu.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!