Wednesday, August 22, 2012

" SINA MPANGO WA KUTOA WIMBO WOWOTE MPAKA NIJIFUNGUE KWANZA "....PIPI


MSANII ambaye siku zinazokuja ataanza kuitwa mama ,Pipi au unaweza kumuita Pipito, amesema kuwa ngoma yake ya ‘Unapokuwa Mbali’ bado inafanya vizuri hivyo sasa atasisima kutoa ngoma hadimpale atakapojifungua.

Pipi
alizungumza na mtandao huu na alisema kuwa kwa sasa yupo kwenye hali ambayo hayawezi kufanya kitu chochote hivyo anaamini baada ya kujifungua atafanya mengi makubwa.

Alisema kuwa anaamini kila mtanzania anahamu ya kazi yake mpya lakini kwa sasa watamsamehe kwani, hata wao wanatakiwa kumuombea ili aweze kukimaliza vyema kipindi cha ujauzito.


“Nina ngoma nyingi ambazo naweza kuzitoa lakini kwa sasa siwezi kufanya chochote kwani ninakalibia kujifungua hivyo nawaomba watanzania wajue kwamba nitakuwa kimya kwa sababu ya hiyo,”
aliongeza
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!