Thursday, August 2, 2012

Snoop Dogg: Mimi ni Bob Marley niliyefufuka!


Allow Snoop to reintroduce himself… his name is Snoop Lion. Sio Snoop Dogg tena! Snoop ameamua kujiingiza kwenye muziki wa reggae kwasababu haoni kama rap ina changamoto tena.


Kwa sasa ameamua kuingia kwa asilimia mia kwenye utamaduni wa raggae na anafanya kazi na producer Diplo kufanya albam mpya ya muziki huo nchini Jamaica.
Snoop ameyaweka matukio hayo yote ya nchini Jamaica kwenye kuisupport albam yake kwenye makala aliyoipa jina la Reincarnated.


Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, Snoop amesema siku zote amekuwa akihisi kuwa yeye ni Bob Marley aliyefufuka.


“I have always said I was Bob Marley reincarnated.” I feel I have always been a Rastafari. I just didn’t have my third eye open, but its wide open right now.”


“Huwa inafika point mtu unasema nimefanya yote ama hakuna mengi ya kufanya tena. Hivi ni kama kuzaliwa kwangu upya.”


Rapper huyo mwenye miaka 40 alisema kuwa kwa sasa amekua mno kufanya rap tena, hivyo anataka kuanza fresh tena. “Rap is not a challenge to me. I had enough of that. It’s not appealing to me no more. I don’t have no challenges. I’m ‘Uncle Snoop’ in rap. When you get to be an uncle, you need to find a new profession so you can start over and be fresh again. I want to be a kid again.”


Muziki wake wa reggae, anauita ‘Muziki wa Reggae wa ukweli.”


Swali ni je! Snoop ataweza kutengeneza rekodi nzuri za reggae kiasi cha kuwa kwenye viatu vya Bob Marley? We shall see that in due time.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!