Thursday, August 23, 2012

SUMA MNAZALETI NA MENEJA MANENO WATIMULIWA "MTANASHATI ENTERTAINMENT"Suma Mnazaleti na aliyekuwa meneja wa Mtanashati Entertainent, Maneno wamefukuzwa Mtanashati Entertainment kutokana na kuonesha utovu wa nidhamu.

Akiongea na Clouds FM kwenye 255 ya XXL leo, mkurugenzi wa kampuni hiyo Ustaadh Juma amesema meneja huyo amekuwa akitumia cheo chake vibaya na pia kuwa na tabia ya kutoa siri za kampuni.

Amesema zaidi ni jana kwenye fainali za kipindi cha Bibi Bomba baada ya meneja huyo kushindwa kufanya kazi yake inavyotakiwa ya kuwaangalia wasanii wake ambao jana walilewa kiasi cha kuiabisha kampuni yake.

Amesema Suma  Mnazaleti amekuwa na tabia chafu kiasi cha kuwaharibu wasanii wake ambapo PNC alikuwa ameacha kunywa pombe lakini tangu Suma ajiunge nao, PNC amerudia kunywa pombe.

Hata hivyo Meneja Maneno ambaye naye amehojiwa amedai kuwa yeye ndiye ameacha kazi baada ya kuona ubabaishaji mwingi kwenye kampuni hiyo.

"Baada ya party ya Bibi Bomba, wasanii wote wametembea kwa mguu wengine mpaka Mwenge, yeye keshachomoka, alichokifanya ni kumchukilia tu Taxi Dogo Janja, halafu leo hii unaondoka unasema wewe ni mtanashati," alisema.

"Meneja huna hata shilingi kumi, unabeep unafanya nini, kwanini nisifanye kazi zangu binafsi. Mimi ndo nimekataa na nimeikataa hiyo Mtanashati lakini naweza nikakuonesha meseji , mimi ndo nimemwambia sitaki sio kwamba yeye ndio kanitumia, hana uwezo wa kunitumia yule mimi."

Wasikilize wote hapa:
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!