Monday, August 27, 2012

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LAWAKUNA WAKAZI WA TANGAWasanii wa Filamu wakionesha Mbwembwe zao jukwaa,Aunt Ezekiel na Shilole.
CMB Prezoo akikamua jukwaani.
Jacob Steven a.k.a JB,mmoja wa wasanii wa filamu nyota hapa nchini akijitokeza jukwaani kuwasalimia wakazi wa Tanga (hawapo pichani),waliofika kwenye tamasha la Fiesta 2012,Mkwakwaani mkoani Tanga.
Jacob Steven a.k.a JB,mmoja wa wasanii wa filamu nyota hapa nchini akicheza muziki laini laini na msanii wa muziki wa kizazi kipya lakini pia ni muigizaji wa filamu,Shilole akiwa ametulia tulii
Sehemu ya washabiki wa tamasha la Fiesta wakishangweka.
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya,CMB Prezoo amabaye pia ni moja wa mastaa waliofanya vyema sana kwenye shindano la BBA 2012,pichani akiwa juu ya jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Dj Zero akiwapandisha mzuka mashabi hawapo pichani 
Palikuwa hapatoshi jukwaaani,shangwe na mayowe zilikuwa zikitawala kila wakati kutoka kwa mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha hilo la Serengeti Fiesta lililofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani,mkoani Tanga.
Kama dawa kama kawa,Msanii Shetta jukwaani akionesha kipaji chake cha kuimba,kucheza na hata kufloo kama wafanyavyo wasanii wengine,
Msanii Ferooz aliyepotea kwenye gemu ya muziki wa kizazi kipya,llakini kwa sasa anarejea kwa kasi,pichani akiwarusha wakazi wa Tanga (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha hilo usiku.
Densaz kutoka nyumba ya vipaji,THT wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Mkwakwani Tanga.
Mwana FA na Linah wakiimba kwa pamoja wimbo wao wa Yalaiti.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mwana FA akishusha misatari ya nguvu jukwaani,mbele ya mamia ya wakzi wa Tanga waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwenye uwanja wa Mkwakwani.==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!