Tuesday, August 21, 2012

"NIPO TAYARI KUWA NA MPENZI ILA SIYO MUME".....AMANDA


MSANII wa filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa hataki kusikia habari ya ndoa kwani ameshaonja uchungu na utamu wake.

Akiongea na waandishi wetu, Amanda alisema kwa sasa hafikirii suala la ndoa na badala yake ataishi katika uhusiano wa kimapenzi tu na mtu kwani ni vigumu kwa mwanamke kukaa bila kuwa na mwanaume.

“Sitaki hata kusikia ndoa kwa sababu nimeshaonja kwa aliyekuwa mume wangu Hamis Bwela kwa hiyo sina wazo kabisa labda itakuja kutokea hapo baadaye lakini kwa sasa ninaweka nguvu zangu katika kazi tu,” alisema Amanda.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!