Monday, August 27, 2012

TEDDY KALONGA AMFAGILIA NGWAIR......ADAI KUWA NI MIONGONI MWA "MARAPER" WAKALI ALIOWAHI KUAFAHAMU
Ghetto Langu, She got a gwan, Kimya Kimya na CNN ni baadhi tu ya nyimbo zinazodhihirisha uwezo mkubwa usio na mfano wa rapper Albelt Mangwea aka Mimi. Sasa hivi anajulikana pia kama CowObama na uwezo wake uko pale pale licha ya kuslow down kiaina.

Nani asiyeujua uwezo wake rapper huyu katika uandishi wa mashairi matata na swag za hatari katika uwasilishaji wa similes na metaphors kwenye ngoma zake? Kwa watanzania waliohamia nchi za nje miaka mitano ama zaidi iliyopita hawajausahau utemi wa rapper huyu mwenye kipaji cha kuchana mitindo huru.

Miongoni mwao ni Teddy Kalonga aka TK, mwanamitindo wa kimataifa, mtangazaji na msanii wa sauti (voice over artist) aishiye Marekani kwa sasa.

Kwake yeye, Ngwair ni miongoni mwa rappers wakali aliowahi kuwafahamu.


“You are one of “The” very few original rappers I know! You are THE |Brand|,” TK alitweet jana kumwambia Ngwair.

@teddykalonga thanks ma’am and I really miss them old days you used to be a great courage … Wanna share with you some new tunes too mami !
— Ngwair (@albertkenneth) August 26, 2012
“Thanks ma’am and I really miss them old days you used to be a great courage … Wanna share with you some new tunes too mami!,” alijibu rapper huyo.

Wawili hawa wanafahamiana vizuri kwakuwa enzi Teddy ni mtangazaji wa Channel 5 walikutana sana katika masuala ya burudani.

Kitu cha msingi Teddy alichoweza kufanya jana ni kujaribu kumuunganisha Ngwair na rapper wa Marekani wa Grand Hustle Records, T.I. kwa tweet hii, “@albertkenneth @Tip I wish you two meet!”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!