Wednesday, August 1, 2012

UNAJUA KATIBA INASEMAJE KUHUSU MADARAKA YA MIHIMILI HII?


Tume ya Mabadiliko ya Katiba,imeshawekwa wazi na imeshaanza kutekeleza mikakati yake katika zoezi gumu na nyeti la uundwaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania. 

Ni zoezi gumu na nyeti sana.Katiba imara,iliyotengenezwa na watu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao kiuchumi,kisiasa na kijamii, ni msingi wa kwanza na ulio muhimu zaidi kama tunataka kuipeleka Tanzania mbele.

Lakini bila kuelewa kilichopo kwenye Katiba Ya Sasa ili kujua nini kiendelee kubakia na nini kiondolewe,hata kama Tume itatumia mabilioni ya dola,mwisho wa siku tutaishia kuwa na Katiba ile ile.Ushiriki wako ni Muhimu.Njia mojawapo muhimu ni kujifunza kwa kuisoma Katiba ya Sasa.

Mojawapo ya maeneo ambayo yameendelea kuwa na mushkeli nchini mwetu ni pamoja na suala la madaraka katika mihimili mitatu mikuu.Kumekuwepo na mijadala kadhaa inayoweka wazi kwamba Rais(kulingana na katiba ya sasa) ana madaraka makubwa kupita kiasi.Ni kweli? Shiriki kwa kuisoma katiba.Bonyeza hapa
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!