Thursday, August 9, 2012

UPDATE: BALOZI COSTA MAHALU ASHINDA KESI YAKE ILIYOKUWA IKIMKABILI

 Aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Italia,Balozi Costa Mahalu ambaye alikua mshitakiwa namba moja kwenye kesi ya matumizi mabaya ya fedha za ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia, pamoja na mshitakiwa namba mbili Grace Martin (kushoto) wakiwa wamezungukwa na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kusomewa kesi yao ambayo wameshinda leo na kuonekana hawana hatia yeyote kutoka na kukosekana kwa ushahidi uliokamilika.
 Balozi Costa Mahalu akiendelea kutoa shukrani kwa Waandishi wa Habari baada ya kushinda kwa kesi yake iliyokuwa ikimkabili.
 Balozi Costa Mahalu akiwasiliana na ndugu na jamaa kwa furaha baada ya kuonekana hana hatia yeyote na kuachiwa huru kuanzia sasa.
Balozi Costa Mahalu (pili kulia) akiwa na Wakili wake,Mabere Marando (kushoto) wakipongezwa na wadau.
 Balozi Costa Mahalu akukumbatiana na ndugu zake.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!