Friday, August 3, 2012

Uruguay yaaga mashindano Olimpiki


Nyota na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez amewashutumu mashabikii wa Uingereza kwa kuizomea timu yake wakati wimbo wa Taifa lake ukitumbuizwa.Mchezaji huyo wa Liverpool alikua mkali na mapokezi kabla ya Uingereza kushinda mechi kwenye uwanja wa Millennium kwa 1-0 dhidi ya Uruguay. 
 Suarez aliongezea kusema kua “bila shaka nasikitika kua tumepoteza na tunarudi nyumbani.”
Kufuatia ushindi wa Uingereza dhidi ya Uruguay sasa nchi hio itapambana na Korea ya kusini mjini Cardiff siku ya jumamosi.

Katika michuano mingine Misri ilijiunga na Brazil katika robo fainali na itachuana na Japan iliyoichapa Belarus 3-1
Washindi wa kundi C Brazil walipata urahisi wa kuishinda New Zealand 3-0 na inatazamia kupambana na Honduras katika hatua ijayo.

Korea ya kusini na Gabon zilishindwa kupasua ngome kwenye uwanja wa Wembley lakini Wa Korea bila shaka waliridhika na pointi iliyowaweka mbele ya Uswizi kuendelea mashindanoni baada ya kushindwa kupata bao dhidi ya Mexico kwenye uwanja wa Millenium.

Brazil iliendeleza rekodi yake ya asili mia 100 ya ushindi ikimaanisha kua Timu hio itaendelea kukaa kaskazini mashariki mwa nchi kwa robo fainali dhidi ya Honduras.
Misri itaondoa kambi hiyo na kuelekea uwanja wa Old Trafford kuzipiga na Japan baada ya mabao ya Mohamed Salah, Marwan Mohsen na Mohamed Aboutrika yaliikosesha Belarus fursa ya kufuzu kusonga mbele kwenye uwanja wa Hampden Park.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!