Saturday, August 18, 2012

UTUMWA WA MAPENZI: LUTENI KALAMA ACHOTESHWA MAJI LIVE HUKU ISABELLA AKITANDIKA BIA......

 ISABELLA NA JINI KABULA

KWELI  mapenzi utumwa! Agosti 13, mwaka huu, saa 10:25 jioni, Kijitonyama jijini Dar, waandishi  wetu waliwanasa wapenzi wawili, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kalama Masoud ‘Luteni Kalama’ na Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda ‘Bela’ ambaye kwa sasa ni mwigizaji wa filamu nchini wakifanya mambo  yaliyozua maswali kwa wapita njia.
 
Waandishi  hao   waliibua maswali baada ya kumuona Bela amekaa nje ya nyumba anayoishi akiwa na shostito wake, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wakinywa bia za baridi tena za chupa huku Kalama akipita mbele yao kwenda kuchota maji nyumba ya pili akitumia ndoo mbili za plastiki kwa kushika huku na huku.

Waandishi hao  wakiwa wamepiga kambi umbali mfupi kutoka walipokuwa watatu hao, walimshuhudia Kalama akipita na ndoo hizo zenye maji akizipeleka kwenye nyumba wanayoishi huku Bela akimwangalia kwa macho yasiyo na chembe ya pole na akiendelea kukata ‘kilaji’ na shosti wake huyo.

Hata hivyo, baadhi  ya wapita njia ambao ni majirani wa wapenzi hao, walidai kuwa, Kalama amekuwa ‘akitumikishwa’ na mrembo huyo kwa kufanya shughuli nyingi za jikoni na hana ujanja kwa vile jamaa anaishi kwa demu hivyo ili maisha yaendelee lazima akubaliane na masharti.


Baada ya waandishi wetu kumshuhudia ‘laivu’ mzee mzima akiteseka, walimwibukia Bela na kumuuliza kuhusu madai kwamba amekuwa ‘akimhenyesha’ mpenzi wake huyo kwa sababu anaishi kwake.

“Acheni hizo, hamjaona watu wanasaidiana kazi? Kama hamjui kusaidiana kazi ni sehemu ya mahabati yetu,” alisema mrembo huyo na kushindilia kinywani glasi ya pombe.  

Waandishi  wetu walipombana Kalama kuhusu madai ya ‘kutumikishwa’ na mpenzi wake huyo, alicheka huku akikataa kuzungumzia tukio hilo akidai yuko bize na kazi na kutaka aachwe mpaka aimalize.


HABARI  HINI KWA  HISANI YA GPL
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!