Monday, August 20, 2012

[VIDEO] :RIHANNA ALILIA PENZI LA CHRIS BROWN

 
 
Kuhusu kupigwa na Chris Brown
Niliumia zaidi. Hakuna mtu aliyejisikia kama nilivyojisikia mimi. Niliumia kwasababu ilinitokea mimi. Ilinitokea mbele ya ulimwengu. Ilinifedhehesha, ilinidhalilisha. Iliuma. 
 
Haikuwa rahisi. Nilimpoteza rafiki  yangu mpendwa. Kila kitu nilichokijua kilibadiika usiku mmoja na sikuweza kuzuia. 
 
Nilitakiwa kukabiliana nacho na sio rahisi kwangu kuelewa ama kutafsiri mbele ya camera wakati dunia ikiangalia. 
 
Kwahiyo ni ngumu kwangu kujali mawazoni mwangu na kutatua mambo kwasababu lilikuja kuwa tukio na najisikia kujilinda.

Nilihisi kama mtu pekee wanayemchukia sasa hivi ni yeye na ilikuwa sehemu ya kushangaza kuwemo. Sababu kwa hasira niliyokuwa nayo, kuumizwa na kusalitiwa, nilidhani alifanya kosa hilo kwasababu alihitaji msaada
 
Nani atakayemsaidia? Hakuna atakayesema kuwa anahitaji msaada. Kila mtu atasema ni mnyama bila hata kuchunguza chanzo. Nilikuwa namjali zaidi.

Kuhusu walivyo sasa na Chris Brown

Tumeurudisha urafiki tena na sasa ni marafiki wa karibu. Tumejenga imani tena. Tunapendana na huenda tutapendana daima. Hicho sio kitu ambacho unaweza kukibadilisha ama kukizima kama umeshawahi kupenda.

Kuhusu iwapo amerudiana na Chris Brown tena

Hapana, yupo kwenye uhusiano wake. Nipo single lakini tumeuendeleza urafiki wa karibu tangu amri ya kutoonana ilipoisha.

Kuhusu tetesi za kwamba walionana St. Tropez, Ufaransa

Ndio nilionana naye. Tulienda kwenye party ya marafiki zetu sote kwenye boti. Ilikuwa noma nilipomuona sababu bado nampenda. Nilijizuia kutoonesha. Nahitaji kuwa hivyo.

Kuhusu kama anadhani Chris Brown ndio mpenzi wake wa kweli

Kabisa. Nadhani alikuwa penzi la maisha yangu. Alikuwa penzi langu la kwanza na naona alinipenda hivyo hivyo. 
 
Tulikuwa wadogo na wa kushtukiza sana. Tulikuwa tunapendana na kukurupuka kiasi cha kujisahau sisi kama mmoja mmoja. Tulisahau kuhusu nidhamu zetu binafsi. 
 
Tulihitaji kitu cha kuzima hilo moja kwa moja na kutuonesha kile tulichokuwa tunakikosa, tulivyokuwa tunachukuliana poa, kujali kila furaha ya mmoja wetu kwahiyo sio tu kitendo cha sisi kuwa pamoja.
 
Nampenda kwa dhati hivyo kitu kikubwa kwangu ni kwamba ana amani. Siwezi kuwa na amani kama hana furaha ama kama bado ni mpweke. Najali. Ni vizuri ameipata hiyo amani.

Kuhusu kama amemsamehe

Nimemsamehe. Ilinichukua muda. Nilikuwa na hasira kwa muda mrefu. Nilijisikia kama hili sio kosa langu lakini bado niliogopa. Nilikuwa na chuki. Nilikuwa na kinyongo. Nilikuwa mweusi na ulikuwa unatoka kwenye muziki wangu na nguo zangu, ulikuwa unatoka kwa vitendo vyangu na sikupenda hisia hiyo. Ilikuwa nzito.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!