Friday, August 24, 2012

"MALAYA WA KUJIUZA WAKO BONGO MOVIE"......HII NI KAULI YA NEY WA MITEGO AMBAYO IMEZUA BIFU ZITO KATI YAKE NA KOLETA

MSANII wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ amejikuta kwenye bifu zito na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’ baada ya kudai kuwa, kijana huyo anatumia bangi.

Akiongea  na  mwandishi wetu , Koleta alisema kuwa kitendo cha Ney kuwachana wasanii wa filamu wa kike kuwa wanajiuza si akili yake bali bangi anayovuta ndiyo inayomtuma kusema hivyo.

 “Ney huenda anavuta bangi tena anatumia mbichi bila kula, huwezi kusema wasanii wa kike tunajiuza wakati huna ushaidi juu ya suala hilo, bangi zake zinampeleka pabaya,” alisema Koleta.

Baada ya kusikia maneno hayo, mwandishi wetu alimtafuta Ney ambaye kwa upande wake alisema: “Huyu dada anatafuta bifu na mimi, niko tayari na simuogopi. Ndani ya wimbo wangu wa Sema Nao ndimo nimetamka maneno hayo sasa kama bangi inanisukuma kusema ukweli, sina sababu ya kuiacha.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!