Monday, August 27, 2012

WADAU WAMPONDA RIHANNA KUMNG'ANG'ANIA CHRISS BROWNBaada ya Rihanna kufunguka kwa Oprah kuhusu penzi lisilokufa kwa Chris Brown – mpenzi wake aliyemdhalilisha kwa kumpiga na kumuumiza vibaya mwaka 2009, ufunuo huo uliwaacha mashabiki wake wengi na mshangao.


Miongoni mwao ni mchekeshaji Joan Rivers, maarufu kwenye kipindi cha Fashion Police cha E! ambaye aliamua kumshambulia Rihanna kwenye Twitter.“Rihanna confessed to Oprah Winfrey that she still loves Chris Brown,” Rivers alitweet.”Idiot! Now it’s MY turn to slap her.”

Rihanna hakukaa kimya na kuamua kumjibu ‘bibi’ huyo mwenye miaka 79.

“@Joan_Rivers wow you really do get slow when you’re old huh?” aliandika Rihanna lakini baadaye aliifuta tweet hiyo.
“Slap on some diapers,” aliongeza Rihanna lakini hii hakuifuta.

“Honey, @Rihanna, everyone knows: If he hit you once, he’ll hit you again,” alitweet bibi huyo. “Read the statistics. PS – Love to have you on Fashion Police!”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!