Sunday, August 19, 2012

WANAMUZIKI 10 MATAJIRI ZAIDI KATIKA BARA LA AFRIKA


Youssou Ndour


1. Youssou Ndour

Huyu ndiye mwanamuziki tajiri zaidi barani Africa. Jamaa anamiliki kituo kikubwa zaidi binafsi cha runinga nchini Senegal, kampuni ya magazeti na kituo chaa radio.

Anamiliki pia night club na record label. Anamiliki kampuni ya nyumba na makazi. Mwaka 2004 jarida la Rolling Stone lilimwelezea kama mwanamuziki maarufu zaidi nchni Senegal na pengine Afrika aliye hai.

Tangu April 2012, ni waziri wa utalii na utamaduni nchini Senegal.

Matumizi ya nyimbo zake yanamuingiza mamia kwa maelfu ya Euro!


2.P-Square

Hakuna msanii wa kizazi cha leo anaeweza kugusa matawi ya mapacha hawa, Peter na Paul Okoye. Wana hela chafu!

Wanachaji dola 250,000 kwa kila show ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 390 za Tanzania! Kuongezea msumari zaidi hapo ni kwamba hawa jamaa wana show kila weekend! Mpaka sasa hivi wameshafanyiwa booking ya kufanya show sehemu mbalimbali duniani hadi March mwakani!

Nyumba yao waliyoipa jina la Squareville huko Ikeja Nigeria ina thamani ya dola milioni 3 ambazo ni zaidi  ya shilingi bilioni 4.

Waliweka historia kwa kuwa wasanii wa kwanza kununua kiwanja kwenye eneo la Banana Island nchini Nigeria ambacho kina thamani ya zaidi ya dola milioni 3 pia!

Wana mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya pili kwa ukubwa ya simu nchini Nigeria ya Globacom wakiwa kama mabalozi wake ambapo hulipwa dola milioni 1 kwa mwaka, wanamiliki pia mijengo kibao ya kupangisha.3.D'banj

Mnigeria huyu aliye chini ya label ya Kanye West, G.O.O.D Music, alitengeneza takriban dola milioni 5 kwenye kampeni ya rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Anamiliki jina la ‘Koko’ linalojumuisha klabu bora za Nigeria za KokoLounge, maji ya kunywa Koko Water na Koko Mobile.

Aliwahi kufanya reality show ya TV  iitwayo Koko Mansion na kulipwa dola milioni 1.

Anamiliki nyumba yenye thamani ya dola milioni 1.5 jijini Atlanta. Ni mwenyekiti mtendaji wa Dbanj Records na pia ana kampuni ya ulinzi iliyofanikiwa sana.

Yeye hucharge dola 100,000 kwa show.

4.Koffi Olomide


Mfalme huyo wa Lingala anacharge tabriban Euro 100,000  kwa show. Jamaa hupiga show nchini Ufaransa zinazojaza karibu watu 80,000  ambapo tiketi moja ni Euro 30 sawa na shilingi elfu 60.

Amekwishatoa albam zaidi ya saba ambazo zimemuingizia mamilioni ya dola.

5.Salif Keita

Anajulikana pia kama ‘Sauti ya dhahabu ya Africa’, ni miogoni mwa watu wanyenyekevu lakini matajiri sana barani Afrika.

Msanii huyo albino anamiliki kisiwa chake binafsi nchini Mali.

Anamiliki majumba na mali zingine nchini Ufaransa na Mali.

6. Fally Ipupa

Msanii huyu anajulikana kama ‘Mfalme mpya wa Lingala’ wa DRC. Kutoka kuwa mcheza show wa zamani wa Koffi Olomide, anasifika kwa kuleta usasa zaidi kwenye muziki wa Lingala.

Ameshakuwa balozi wa brand nyingi za nguo nchini Ufaransa, concerts zenye gharama na kuuza kopi kibao za albam zake.


7.2 Face Idibia


Msanii huyu wa Nigeria anamiliki nyumba za kupangisha zenye gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.

Hulipwa kuanzia dola 50,000 - 80,000 kwa show.

Anamiliki pia klabu ya usiku ya nguvu na biashara zingine zinazomuingizia hela nyingi.

8.Hugh Masekela


Huyu ni miongoni mwa wanamuziki wa Jazz wanaoheshimika zaidi barani Africa.  Anamiliki mobile studio yenye mafanikio makubwa nchini Botswana. Hushiriki kwenye matamasha makubwa duniani na huingiza mamilioni ya dola kutokana na mauzo ya albam zake.

9. Banky W

Anajulikana kama Mr. Capable pia. Banky W hufanya show mara tatu ama nne kwa wiki zinazomuingiza mshiko mrefu mno. Aliwahi kuwa balozi wa kampuni ya simu ya Estisalat ya Nigeria ambapo alitumika kwenye matangazo yake.

Kwa sasa ni balozi wa Samsung Mobile. Amewahi kufanya kampeni ya Coca Cola-Nigeria na Microsoft’s Anti-cyber Crime Initiative.

Kutokana na kuingiza hela nyingi amenzisha mradi kuwasaidia wasiojiweza kwa kuwalipia ada watoto wenye uwezo darasani chini ya Mr. Capable Foundation.

10.Chameleone

Mzee wa Valuvalu anafunga list kwa kuwa msanii mwenye hela zaidi kuliko wote Afrika Mashariki.

Anamiliki gari Cadillac Escalade yenye thamani kubwa, Mercedes Benz ML 320,  Super Custom, convertible na Premio.

Anaishi kwenye nyumba yenye gharama kwenye maeneo  ya wazito huko Seguku Hill kwenye viunga vya Kampala, simu zake mwenyewe na mali zingine nyingi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!