Thursday, August 2, 2012

WAREMBO WAKALI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI


Mtandao wa Vibeweekly.com wa Kenya umeandika makala iliyoipa jina la ‘East Africa’s Most Beautiful Female Celebrities’.

Makala hiyo kwa mujibu wa mtandao huo imewaangalia wasichana kumi mastaa warembo zaidi Afrika Mashariki. 


Hata hivyo list hiyo ya warembo hao imetawaliwa na wanawake wa Kenya kiasi ambacho kinaifanya isiwe na hadhi ya kuwa chart ya Afrika Mashariki yote.

Cha kustaajabisha,kuna warembo wawili tu wa Uganda na mmoja wa Tanzania ambaye ni Vanessa Mdee.
Kwa upande wa Uganda, makala hiyo ina kasoro kubwa kwa kutomjumuisha mwanamke mrembo kuliko wote nchini Uganda kwa mujibu wa kura nyingi zilizopigwa mwaka jana, Zari Hassan.


Hawa ndio wanawake warembo zaidi Afrika Mashariki kwa mujibu wa mtandao huo.
1.Juliana Kanyomozi – Uganda
Mwamamuziki na jaji wa Tusker Project Fame.

2.Sharon O – Uganda
Mshiriki wa Big Brother Africa Season 6 na member wa kundi la Obsessions.

3.Julie Gichuru – Kenya
Msomaji wa habari wa kituo cha runinga cha Citizen nchini Kenya.

4.Sheila Mwanyigha aka Nikki – Kenya
Mwanamuziki na mtangazaji wa TPF.

5.Anne Kiguta – Kenya
Msomaji wa habari wa KTN Prime Time News.

6.Kambua – Kenya
Muimbaji wa muziki wa injili na mtangazaji mwenza wa kipindi cha ‘Rauka’ cha Citizen Tv.

7.Lilian Muli – Kenya
Msomaji wa habari wa Citizen TV.

8.Joey Muthengi – Kenya
Channel O VJ/Rapper/Capital FM presenter.

9.Alice Kamande – Kenya
Mc na mwanamuziki wa gospel.

10.Vanessa Mdee – Tanzania
Mtangazaji wa MTV Base na Choice Fm Tanzania.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!