Monday, August 27, 2012

WASANII WA KIMATAIFA WAENDELEA KUMIMINIKA NCHINI UGANDA

Wasanii wa dancehall kutoka Jamaica, Sean Paul na Spence a.k.a Konshens hivi karibuni wanatarajiwa kutumbuiza nchini Uganda.

Vyanzo nchini humo vimedai kuwa Koshens ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wasanii maarufu nchini Jamaica ataperformi  live jijini Kampala October 5,2012 na baada ya mwezi mmoja Sean Paul anatarajia kurudi tena Kampala kuangusha show.
 
Wakati huo huo Jumamosi hii mwanamuziki wa Marekani wa kundi la Dru Hill aliyetamba na ngoma kama ‘Unleash the Dragon’ Sisqo amepiga show ya nguvu jijini humo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu.

Show hiyo iliyokuwa ana ulinzi mkali imeshuhudia polisi zaidi ya 2,000 wakisambazwa kulinda usalama kwenye show hiyo.

Sisqo, ametumbuiza na msanii wa Ghana Fuse ODG wa Azonto Dance.

Wasanii wa Uganda waliosindikiza show hiyo ni pamoja na Jose Chameleone, Bobi Wine na Jackie Chandiru.

Wiki moja tu iliyopita wajamaica wengine Demarco na Wayne Wonder walikuwa nchini humo kutumbuiza.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!