Saturday, September 1, 2012

"VIDEO YA PETE SIIFANYII HAPA BONGO".........BEN POLMuimbaji mahiri wa Bongo Flava, Ben Pol jana amesema kwa namna yoyote ile, video ya wimbo wake mpya uliotoka wiki iliyopita, Pete, lazima aifanyie nje ya nchi. Pete ni wimbo wa kwanza tangu ajiondoe kutoka kwenye label yake ya awali ya M-LAB.


Ben Pol ameonekana kuifuata idea ya mwenzake, Ommy Dimpoz aliyesafiri hadi nchini Afrika Kusini kufanya video yake ya Baadaye.

“South Africa ni wazo la kwanza tu lililokuja, kwahiyo chochote tunaweza tukafikiria lakini, kimsingi video yake haitashutiwa hapa,” Ben Pol aliiambia Power Jams ya East Africa Radio.


Amesema video hiyo anaweza kuifanya na Ogopa Djs jijini Nairobi, Kenya ama Adam Juma wa Visual Lab ambaye watasafiri naye hadi Afrika Kusini.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!