Friday, September 28, 2012

AUNT LULU AKIRI KUWA YEYE NI SAWA NA DARAJA LA WANAUMESTAA wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ ametoa la moyoni kuwa, anaumizwa na kitendo cha baadhi ya wanaume kumtumia kimwili kisha kumtosa.

Akizungumza kwa masikitiko hivi karibuni, Aunty Lulu alisema yeye ni mwanamke anayehitaji mpenzi mwenye nia ya kumuoa lakini anashangaa kila anayekuwa naye anamtumia kama daraja kisha akifanikisha mambo yake anampotezea.


“Wananifanya mimi ni daraja. Wanapita kwangu ili kufikia malengo yao, wakiona wamefanikiwa wanaanza chokochoko ili tuachane, inaniuma sana,”
alisema Aunty Lulu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!