Saturday, September 8, 2012

AY AJIPANGA KUNUNUA NYUMBA NA KUANZISHA BIASHARA ZAKE KIBAO NCHINI KENYA


Mtandao wa Ghafla wa nchini Kenya jana uliandika habari inayodai kuwa huenda msanii wa Tanzania aliyetajwa kwenye tuzo za Channel O 2012, Ambwene Yesaya, akahamia jijini Nairobi, Kenya.


“Seeing that Nairobi is kind of like the center of all showbiz matters in East Africa, AY has seen it convenient and advantageous to set up shop here in Nairobi. According to sources, AY was actually looking for a vacant office days before he left for his country.


Could he be the next artist to relocate to Kenya? I sure hope so,” uliandika mtandao huo.


Mwandishi aliamua kumpigia simu AY ili kumuuliza kama kweli ana mpango wa kuhamia nchini Kenya na kufungua duka.

“Unajua sehemu unaenda sana sana, unakaa sana mahotelini, so why unakaa hotelini si uchukue apartment tu? Lakini sio kwamba kusema eti nahamia, hii the way navyoenda tu nahitaji kukaa sehemu ambayo ni permanent,”alisema. 


Kuhusu aina ya biashara atakayofanya jijini Nairobi AY alisema, “Unajua hizi biashara zetu, shop, club , pub, yaani vitu ambavyo vinazunguka mazingira yetu, huwezi kusema yaani hapa hapa nifungue duka la spea za magari, labda uwe na uzoefu na hiyo side lakini kama huna uzoefu na vitu kama hivyo ni bora ucheze na vitu ambavyo vinakuzunguka.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!