Monday, September 10, 2012

BAADA YA DIAMOND SASA NI ZAMU YA HAFSA KAZINJA KUPIGA SHOW NCHINI MAREKANI

Baada ya Diamond kufanya show kali ya 3hrs nonstop akiwa na vijana wake wa Wasafi nchini marekani September mosi ya mwaka 2012, sasa ni zamu ya bibie anayefanya muziki wa Zouk aliyewahi kutamba na hit song yake ya Presha, Hafsa mwana wa Kazinja.   

Akiongea na Mpekuzi, CEO na President wa Kampuni ya J & P Entertainment bwana Peter Ligate,  amesema Hafsa Kazinja anategemewa kufanya show yake tarehe 22 september 2012 in the US, na kuwahamasisha mashabiki wote wa muziki wa zouk wa Afrika mashariki walioko Marekani kuhudhuria kwa wingi.

Peter Ligate
Peter Ligate ni mtanzania anayeishi marekani, ambaye amekua mstari wa mbele katika ku upromote muziki wa bongo nchini humo kwa kuandaa maonesho na kuwaleta wasanii mbalimbali wa bongo. 

Baadhi ya wasanii ambao Ligate chini ya J & P  amewahi kufanya nao shows nchini humo ni pamoja na Ali Kiba, Mr Nice, Khadija Kopa, Linah, Diamond na hivi sasa Hafsa Kazinja.

Diamond Epic show Washington DC 1st Sept 2012
Pia Ligate ameongeza kuwa baada ya Diamond Platnums kufanya show 1 ya utambulisho na kurejea nyumbani Tanzania, anategemewa kurudi tena US hivi karibuni kwa ajili ya tour waliyoipa jina la DIAMONDS R FOREVER US TOUR.

Hard working pays, hii ni changamoto kwa wasanii wote kama mtajituma then you will be recognised anywhere. Keep it up guys.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!