Wednesday, September 19, 2012

BAADA YA KUTOHUSISHWA KWA MIAKA MITANO MFULULIZO, T.I.D AILILIA FIESTA


Ukiona mwanaume ka express feelings zake kwa uchungu basi ujue kaumia sana. 
 
 Jumanne 18th Sept 2012, kupitia akaunti yake ya facebook yenye jina “Topindar Tid Top band”, msanii wa R&B wa Tanzania Khalid Mohamed anaefahamika kwa jina la muziki kama TID, amaeamua kufunguka na kuelezea yake ya moyoni juu ya kuumia kwake kwa kutokuwepo katika list ya wasanii wanaoshiriki katika  shows za tamasha la Fiesta ambazo zinaendelea katika baadhi ya mikoa ya Tanzania. 

Tid anaamini kuwa yeye ana deserve kuwemo katika orodha hiyo, lakini anaamini kuna watu wanafanya jitihada za kumfanya aonekane hastahili kuwepo katika orodha hiyo na akaongeza kuwa huu ni mwaka wa 5 hajahusishwa katika tamasha hilo.

Hii ndio status ya T.I.D:

“I wiSh I coUld maKe the Guy Who does the FieSta Listing be oN my SiDe some PeoplE are workin verY Hard to juSt makE me Look like Criminal so I can not be on List Lakini Mungu atanipa Better than Fiesta tho its Been 5 years am nt Part of It”


Baadhi ya wasanii ambao wako katika list ya Fiesta ya mwaka huu ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz,  shetta, Juma Nature, Recho, Nuru, Stamina, Ferooz, Linah, Mwana FA, Joh Makini, God Zilla na wengine wengi.

Hili ni tamasha kubwa la muziki ambalo hufanyika kila mwaka, na huandaliwa na moja ya radio kubwa hapa nchini Clouds Fm, na huzunguka katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani. Wiki hii Fiesta inaelekea Iringa na Mbeya.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!