Friday, September 14, 2012

BELLE 9 APIGA COLLABO NA WASANII KUTOKA MAREKANI.....ADAI KUWA ANA MPANGO WA KUJULIKANA KIMATAIFA


Mbali na wasanii hao wa Marekani pia Belly 9 alisema kuwa ameshafanya collabo nyingine na wasanii kama Nazizi kutoka Kenya na Cannibal huku akiamini kuwa kuvuka mipaka ya kufanya kazi na wasanii hao kunaweza kufungua njia nyingine ya kufika mbali zaidi.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na ngoma nyingine mpya inachokwenda kwa jina la ‘Anayeishi naye’, ambayo ndani yake anapatikana kijana Ben Pol, wakati ngoma zake kama Amerudi’, ‘Suma ya Penzi’, ‘Masogange’ bado zinafanya vizuri.

“Malengo yangu ni kutoka kimataifa kwani nafanya muziki ili nao uniweke kwenye nafasi fulani kimaisha, muziki ni ngumu pale unapoufanya kama mchezo lakini unakuwa mzuri pale unapoufanya kwa malengo na kujua ni kazi hivyo kwa upande wangu nalenga kufika mbali zaidi,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa hana mpango wowote wa kutoa albamu kwa mwaka huu, kwani tatizo kubwa linalomuumiza ni pale watu wanapotumia njia za mkato kama ku-burn albamu ya msanii huku wakisahau kuwa wao wanatumia gharamu nyingi za pesa na muda katika kutengeneza wimbo hadi unakuja kukamilika na kwenda sokoni.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!