Wednesday, September 12, 2012

"NDOA BILA KAZI IMENISHINDA"- AMANDA.MWIGIZAJI wa filamu mwenye jina kubwa , Amanda Poshi amefunguka kuhusu kutalikiana na aliyekuwa mumewe Hamis Bwela ambaye aliachana naye siku za karibuni kutokana na sababu ya mumewe kumzuia asifanye kazi yoyote zaidi ya kukaa ndani tu na kama akitoka wawe sote.

Amanda Poshi
Amanda Poshi

“Ndoa imenishinda aliyekuwa mume wangu alikuwa hataki kabisa nifanye kazi yoyote zaidi ya kukaa ndani tu, maisha ya sasa si maisha ya kusubiri uletewe kila kitu lazima mwanamke uhangaike na si kuwa tegemezi sasa mtu ukae ndani tu kama mwali au mwanamke wa mwarabu maisha ya sasa,”anasema Amanda.

Amanda amedai kuwa mumewe alipomuoa alijua kuwa yeye ni mwanamke mjasiriamali ambaye pamoja na kufanya shughuli zake ndogo ndogo lakini kazi yake kubwa ni uigizaji ambayo anaamini kuwa inawezekana hata mumewe huyo alimwona kupitia filamu na tamthilia na kumpenda awe mkewe iweje amzuie asifanye kazi yoyote?
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!