Wednesday, September 12, 2012

BONGO MOVIE: LUCY KOMBA AIRITHI MIKOBA YA KANUMBA BAADA YA KUTAMBA NCHINI GHANA NA SIERRA LEONE


Bongo movie  inazidi  kujiimarisha  vyema nje  ya  nchi.


Baada ya marehemu Steven Kanumba kufungua njia saivi ni zamu ya mwanadada Lucy Komba. Habari  za  kuaminika ni kwamba mwanadada huyo ameingia makubalino na aliyekuwa International manager wa The late Kanumba, Mr.Richard Nwaobi, ambaye pia ni manager wa Rose Ndauka.


Hivi karibuni ,Lucy alikwea  pipa kuelekea  Ghana ambapo alienda kushoot movie ambayo ilikuwa imepangwa arekodi na Kanumba.

 Katika hali ya kuthibitisha ukweli , Lucy  anafunguka  kama  ifatavyo: “Nilivyoenda Ghana nikapata nafasi ya kufanya movie nyingine nchini Searra Leone, movie yenyewe imeshakamilika na wana-plan ya kuifanyia uzinduzi kwenye nchi zote ambazo washiriki wanatoka. 

Movie inaitwa Repackage live. So nimefanya movie mbili, moja imeshakamilika na nyingine bado wanatafuta mbadala wa Steven Kanumba”.


Lucy Komba pia amefanya appearance kwenye famous film magazine in Africa, ambayo imewa-feature mastaa kama Van Vicker, Ini Edo na wengine kibao. Kutoka Bongo walihusishwa Steven Kanumba na Lucy Komba tu.


“All publicity inasababishwa na manager wangu Mr Richard Nwaobi, magazine inaitwa Filmbiz. Inasambazwa Africa nzima na Ulaya. 

Content yake is all about African movies na mastaa wake, wameniuliza mengi kuhusu Bongomovie and I belive watakuja kufanya na mastaa wengine pia- Lucy Komba.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!