Thursday, September 20, 2012

CAMP MULLA KUTOKA KENYA WAMEKUWA NOMINATED KATIKA MOBO AWARDS 2012 UK


Camp Mulla


Kundi lenye swag za kutosha kutoka nchini Kenya linalofahamika kama Camp Mulla, limeendelea kuiwakilisha nchi yao vizuri kimataifa baada ya kuwa nominated katika awards za MOBO zinazotegemewa kuchukua nafasi mwezi November 2012 huko Liverpool, Uingereza.

Kundi hilo la Camp mulla lenye members watano, na mmoja kati yao akiwa ni first lady, limefanikiwa kuingia katika award hizo katika category ya Best African Act.

Wasanii wengine kutoka mataifa mengine ya Africa ambao wamekuwa nominated katika Mobo Awards ni pamoja na P-Square, Fally Ipupa, D’banj, Cabo Snoop na wengine.

Hizi ni Tuzo za 17 toka Mobo ilianzishwe mwaka 1996 huko Uingereza, zikiwa na lengo la kutambua mafanikio makubwa wanayoyapata wanamuziki mbalimbali wa bara la Africa .
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!