Thursday, September 27, 2012

CHARLES BABA AWAPA MAKAVU WASANII WA BONGO FLEVA


STAA wa Bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amefunguka kuwa anawachukia sana wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kwa madai kwamba  wanaharibu tasnia nzima ya muziki nchini.
 
Akichonga na Mpekuzi, Chaz alisema wasanii hao wanabebwa kwa aina ya muziki wanaoimba tofauti na wale wa dansi ambao wanajua nini maana ya muziki na wanaimba ‘live’ bila kutumia CD kama wafanyavyo Bongo Fleva.

“Mimi kutoka rohoni nawachukia sana wasanii wa Bongo Fleva, huwa naongea nao basi tu kwani ndiyo wanaotuharibia muziki, mtu anakwenda kurekodi wimbo mmoja akishasikika anajiita mwanamuziki kumbe hakuna kitu, ” alisema Chaz.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!