Friday, September 14, 2012

"NILIMPIGA CHINI IRENE UWOYA KWA SABABU ALITOA MIMBA YANGU"....H.BABABaada ya kukaa kimya kwa muda muda mrefu tangu Irene Uwoya amchafue mpenzi wake wa zamani, H.Baba kuwa hana lolote kitandani, msanii huyo wa Bongo Flava ameamua kusema sababu halisi ya kuvunjika kwa uhusiano wao.


Akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds FM , kwa sauti iliyoonesha wazi ghadhabu ndani yake, H.Baba alisimulia kuwa alimpa ujauzito Irene na kumsisitiza kuwa asiitoe kwakuwa angependa kuwa na mtoto. 

Alisema siku moja Irene alimwambia mpenzi wake huyo wa zamani kuwa anajisikia vibaya hivyo akampeleka dispensary kuchukua vipimo ili aanze dozi.


H. Baba ambaye jina lake la kwanza ni Hamis, alidai kuwa baada ya kufika hospitali na Irene kumuona daktari, alishangaa kuona kuwa mpenzi wake amekaa kwa muda mrefu kwenye chumba cha daktari. 

Alisema alipotoka, Irene alionekana amelegea isivyo kawaida na ndipo (Irene) alipomwambia ukweli kuwa amechomoa mimba.

Kitendo hicho kilimuumiza Hamis ambaye alidai kuwa kila mmoja alirudi nyumbani na njia yake na huo ndio ukawa mwisho wa penzi lao.

Alisema kilichomkera zaidi ni kuwa, Irene aliandika jina lake (Hamis) kwenye kadi ya hospitali. “Je kama angekufa ingekuwaje?” alisema H.Baba.

Kutokana na maelezo hayo, vita vya maneno kati ya wapenzi hao wa zamani ndio kama vimeanza tena. Tutegemee mazito hivi karibuni kutoka kwa Irene Uwoya.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!