Friday, September 14, 2012

CHOCOLATE YA ODAMA INAPATIKANA SOKONI KUANZIA LEO

Ile filamu iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu toka kwa Jennifer Kyaka alias Odama ikiwa imetengenezwa chini ya kampuni yake kwa jina la J-Film 4 Life imeingia sokoni siku ya leo.

Habari toka kwa wasambazaji wa filamu hiyo ambao ni Steps Entertainment LTD ni kuwa filamu hiyo ipo sokoni siku ya leo tarehe 14 September, hivyo wapenzi wa Odama wanaweza kwenda dukani na kujipatia copy zao nakuweza kuona uwezo mkubwa uliofanywa na wasanii waliocheza movie hiyo toka kiwanda cha Swahiliwood.

Kwenye Movie hiyo ya Chocolate utapata kuwaona  wasanii nguli katika tasnia hiyo kama Yusuph Mlela, Odama mwenyewe, Jacqueline Wolper na wengine wengi.
Check out baadhi ya vipande vya movie hiyo:


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!