Monday, September 24, 2012

COLLABO YA AVRIL WA KENYA NA AT YASHINDIKANA BAADA YA MWADADA HUYO KUISHINDWA STYLE YA AT

Avril Nyambura
Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya, Avril Nyambura hivi karibuni ameshindwa kumridhisha AT kwa kiwango chake cha uimbaji baada ya msanii huyo mahiri kwa mduara kutaka kumpa collabo.

Akiongea na Mpekuzi, AT amesema alisafiri hadi jijini Nairobi na kukutana na Avril kwenye studio za Ogopa DJ, na kumwandikia mashairi na melody msanii huyo ambazo hata hivyo zilimshinda kuziimba.
AT
Ameongeza kuwa pamoja na kurudia sana sauti hizo, Avril alishindwa na hivyo AT aliamua kumpa muda zaidi wa kuifanyia mazoezi ili aje kuifanya baadaye lakini hata hivyo kazi hiyo haikufanyika tena.

Awali AT amedai alikuwa amepanga kufanya wimbo na Juliana wa Uganda na alienda kumtafuta hadi nchini kwake lakini hakufanikiwa kumpata.

Amesema imembidi amtafute msichana aitwaye Alice wa THT ambaye ameweka vionjo vizuri zaidi kuliko alivyokuwa akitegemea.

Wimbo huo anaosema una mahadhi ya zouk classic utatoka mwezi ujao na amepanga kufanya video kali.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!