Saturday, September 29, 2012

DEMU WA MR. BLUE AJIPANGA KUINGIA BONGO MOVIE

Hitmaker wa Don’t Let me Go, Naj, anatarajia kujiingiza kwenye filamu baada ya kumaliza masomo yake nchini Uingereza.

Najma ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na Mr. Blue na kuonekana kwenye video ya mkali huyo ‘Tabasamu’, pamoja na kumshirikisha kwenye ngoma yake Don’t let me go, amesema masomo yalikuwa yamembana zaidi na kwakuwa sasa amemaliza yupo tayari kuendelea na muziki pamoja na kuingia rasmi kwenye uigizaji wa filamu.

Akiongea na kipindi cha Friday Night Live cha EATV jana, mrembo huyo amesema japo hawajui waigizaji wengi wa Bongo Movies, amesema anachoamini ni kuwa anaweza na anapenda kuigiza hivyo ni kitu ambacho lazima akifanye.

Mwezi June mwaka huu, Naj aliachia video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha AY, Let’s Dance.

Aliongeza kuwa hivi karibuni ataachia ngoma yake mpya aliomshirikisha ex wake Kabayser na Dully Sykes
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!