Monday, September 10, 2012

DIAMOND NA MPENZI WAKE WEMA SEPETU WATARAJIWA KUPIGA SHOW YA NGUVU MALINDI KENYACouple maarufu nchini Tanzania inayofananishwa na ile iliyovunjika na inayotaka kurejea ya Chris Brown na Rihanna, ya Diamond na Wema Sepetu, inatarajiwa kupiga  show  mjini Malindi, Kenya hivi karibuni.


Kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya, Diamond ambaye jina lake halisi ni Abdul Naseeb, ataongozana na mwandani wake Wema Sepetu kwenye show itakayofanyika Club Pata Pata mjini Malindi.


Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa hitmaker huyo wa Mawazo, mjini Malindi.

Taarifa hizo zimetolewa na mkurugenzi wa klabu hiyo Fedele Grasi.


Tarehe 1 mwezi huu Diamond alipiga show ya nguvu mjini Washington DC, Marekani japo hakuongozana na Wema ambaye alikuwa kwenye tour ya Fiesta na wasanii wengine wa Bongo movies.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!