Friday, September 14, 2012

D.N.A KUTINGA MAHAKAMANI JUMATATU IJAYO


Rapper D.N.A toka pande za area code 254 ambaye aliibamba vya kutosha music scene ya Afrika Mashariki kwa ngoma yake ya “Banjuka” na sasa anatamba na single yake kwa jina la “Maswali ya polisi“  atafika mahakamani siku ya Jumatatu kwenye case aliyoishitaki Bank maarufu huko Kenya kwa kitendo chao cha kutumia parts za track hiyo kwenye tangazo bila ridhaa yake.

D.N.A anataka alipwe kutokana na hasara ambazo Bank hiyo imemsababishia kwa alichokiita ‘overstepping on his patents‘. Pia D.N.A ana-claim kuwa kampeni ya Bank hiyo ambayo inawalenga vijana,  inawafaidisha sana wao kupitia wimbo wake huo. Hata tittle ya campaign hiyo ina jina la wimbo huo wa D.N.A.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!