Tuesday, September 4, 2012

DOGO JANJA AENDELEA KUNYANYASWA....TUNDAMAN ATAKA CHORUS YAKE IFUTWE NA MANECKY NAYE AMUITA "SNITCH"Jumapili na Jumatatu hii zilikuwa chungu kama shubiri kwa Dogo Janja baada ya washkaji zake wa zamani kumpa makavu live!


Jumapili Dogo Janja alipiga show yake kubwa jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Maisha Club ya kwanza tangu ajiunge na Mtanashati Entertainment. 

Hata hivyo siku yake iliharibika baada ya kukutana na producer Manecky wa AM Records ambaye tayari alikuwa amechangamka na bia mbili tatu kichwani.


“Nilipanda VIP nikakutana na Manecky, Manecy producer nikamsalimia…. Akaniambia siongei na masnitch, nikamwambia bro kwani kuna nini? Akaanza kunitukana matusi ya nguoni yaani kanitukana sana mpaka nikajisikia mpweke yaani halafu yeye alikuwa amelewa,” Dogo Janja aliambia Power Jams ya East Africa Radio jana.

“Ikabidi nishuke chini nikapanda juu nikakutana na Tunda, Tunda nilikuwa nasalimiana naye vizuri, tena Manecky akaanza kunitukana nikajua labda ni pombe”

Alisema baada ya kuona hivyo alienda kuongea na bosi wake Ustadh Juma kuhusu tukio hilo ambaye alienda kwa Manecky kumuuliza sababu ya kufanya hivyo. 

Akiwa amelewa, Manecky aliendelea kulaumu na kudai kuwa alichukia kitendo cha Dogo Janja kwenda kufanya wimbo na Marco Chali.

Kama haitoshi jana alipigiwa simu na Tunda Man ambaye naye alikuja na lake, akimtaka afute sauti zake zote zinazosikika kwenye nyimbo za Dogo Janja walizofanya collabo.


“Sasa mimi cha kushangaza leo napokea simu, Tunda anasema kwamba nifute chorus ya ‘Anajua’.

 Lakini sasa mimi nashangaa sababu ile nyimbo ya Anajua, nimerekodi.. na kipindi nafanya kazi ya Tip Top nilikuwa nafanya kazi kwa moyo mmoja na nilikuwa naithamini kazi yangu, nilikuwa na mapenzi na kazi yangu na nilijitahidi nikafanya kazi nzuri, watanzania wakaipokea vizuri wakamwelewa Dogo Janja”

Amesema hata hivyo hawezi kuzifuta sauti hizo kwakuwa ni haki yake.


Sitofuta ile nyimbo sababu ni mali yangu na Tunda mimi nimemshirikisha. Mbona Tunda anafanya collabo na akina Shettah ile chorus ya Mdananda, kapiga nyimbo na Pasha, mbona hamuambii Pasha afute nafasi yake, ananiambia mimi nifute sababu mimi mdogo labda, ” alisema Dogo Janja kwa uchungu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!