Thursday, September 27, 2012

DULLY SYKES AJIPANGA KUJA NA KAMPUNI YAKE YA VIDEO PRODUCTION


Mr Misifa Dully Sykes amesema kuwa anampango wa kufungua kampuni yake mwenyewe ya kutengeneza Video baada ya kumiliki audio studio ya Dhahabu records kwa miaka kadhaa sasa.

Dully kupitia website yake ameandika: "Mashabiki wangu nawapa nafasi ya pekee ya kuchagua jina la kampuni yangu mpya ya Video Production inayotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni. Tupia jina kwenye comments."  

Hapo kabla Tumeshuhudia wasanii wengi wa hapa bongo wakifungua music production studios zao wenyewe na kufanya idadi ya audio studios zinazo exist izidi kwenda juu. 


Mpaka sasa wasanii wanaomiliki studio zao wenyewe za audio ni pamoja na Dully Sykes, Juma nature, Said Fella, Mike Tee, Benja wa Mambo Jambo na wengine.

Sasa naona kete inahamia kwenye video production, msanii ambae ameshaanza kufanya kazi kama producer kupitia kampuni yake mwenyewe ya kutengeneza videos ni Benjamin wa Mambo Jambo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!